WADAU WALALAMIKIA WATUMISHI TRA
Wadau wa kodi nchini, wamewalalamikia baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutotenda haki wakati wa ukadiriaji wa kodi kwa wafanyabiashara.
Wakitoa maoni yao baada ya mamlaka hiyo kutangaza ofisi zao zitafanya kazi nchi nzima leo Jumamosi, wadau wamesema baadhi ya watumishi hao hukadiria kodi kubwa kwa baadhi ya wafannyabiashara bila kuwauliza.
"Utakuta llabda una kiduka chako, anakuja tu anakadiria kodi ambayo inakushangaza hata wewe mwenyewe maana biashara ngumu sana. Basi ni bora hata akuulize umweleze biashara ilivyo," alisema Dismas Disman mwenye duka la mbao.
Mfanyabiashara mwingine aliyeomba hifadhi ya jina lake akisema hapo baadhi ya maduka makubwa yanalipa kodi ndogo huku maduka madogo yakilipa kodi kubwa.

Post a Comment