MUSEVENI ASHANGAA KINACHOWAVUTIA WANAUME KWA WANAUME WENZAO
Wakati Jumuia ya kimataifa ikipigia upatu ndoa za jinsia moja kwa kigezo dhaifu cha haki za binadamu, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameonyesha mshangao wa kipi hasa kinachowavutia wanaume kwa wanaume wenzao.
Katika kipande cha video kinachosambaa mitandaoni, kiongozi huyo wa muda mrefu nchini Uganda, alisema bado hafahamu hasa ni nini kinapelekea mwanaume kumuoa mwanaume mwenzake.
"Hata sasa sifahamu, unashindwa kuvutiwa na warembo lakini unavutiwa na mwanaume mwenzako? Ni jambo zito sana, inamaanisha kitu fulani hakiko sawa akilini mwako."

Post a Comment