DIAMOND AONEKANA CLUB LONDON AKIWA NA CHRISS BROWN, WATABIRIWA COLABO

Nyota mkubwa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz ameonekana katika klabu moja ya usiku jijini London akiwa na mwanamuziki maarufu wa Marekani, Chriss Brown.

Chriss, mmoja kati ya wanamuziki watukutu nchini Marekani, alionekana katika video iliyopatikana katika akaunti ya instagram ya Diamond akiwa pamoja na meneja wa msanii huyo wa Bomgo, Sallam SK.


Ingawa hakukuwa na maelezo yoyote zaidi ya video hiyo, upo uwezekano mkubwa wa wawili hao kufanya kazi kwani imekuwa ni kawaida kwa kijana huyo wa Tandale kutopoteza nafasi anapokutana na msanii mkubwa.

Kabla ya Chrisss, Diamond pia ameshafanya kazi na wasanii wawili wakubwa wa Marekani, Neyo na Marion.


No comments