WABUNGE WAUSHITUKIA MKATABA WA LIGANGA NA MCHUCHUMA
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo wamechachamaa kuhusiana na mkataba katika migodi ya makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma, wakidai ni wa kifisadi.
Wakichangia ripoti ya kamati iliyoundwa kuchunguza mkataba huo, wabunge hao walishangazwa ni kwa namna gani, ulimwezesha mwekezaji huyo mwenye fedha ndogo, kuweza kupewa mradi huo wa mabilioni ya dola.
Kwa mujibu wa wachumi, mradi huo una makaa ya mawe unaokaridiliwa kuwa na thamani ya dola bilioni tatu.
Waziri anayehusika na uwekezaji na viwanda, alisema serikali itaifanyia kazi ushauri wa wabunge kuhakikisha nchi inanufaika na mkataba huo.

Post a Comment