TSHISEKEDI AISHTAKI DUNIA KWA PAPA FRANCIS
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi ameishtaki dunia mbele ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa kile kinachoendelea nchini kwake.
Tshisekedi alimwambia Papa kuwa dunia imekaa kimya bila kuchukua hatua wakati mapigano ya waasi yanayosaidiwa na nchi jirani yakiendelea huku mamia ya wananchi wake wakipoteza maisha na wengine wakipata vilema vya maisha.
Nchini DRC, kumekuwa na mapigano ya vikosi vya waasi wakiongozwa na M23, ambao wanadaiwa kusaidiwa na nchi jirani ya Rwanda.
Uganda nayo pia inadaiwa kuwasaidia waasi ambao wanadaiwa kugombea machimbo ya dhahabu ambayo inapatikana kwa wingi nchini humo.

Post a Comment