YANGA YALAMBA DILI NENE KOMBE LA SHIRIKISHO
Klabu ya soka ya Yanga, imeingia mkataba wa mamilioni ya shilingi na Kampuni ya vifaa vya umeme ya Haier0 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Jina la kampuni hiyo litakaa mbele kifuani, kuchukua nafasi ya mdhamini wao wa miaka mingi, SPOTPESA ambao kanuni za Shirikisho la soka Afrika zinawakataa.
Bosi wa GSM, Ghalib Said Mohamed akifuatilia utiaji wa saini
Kanuni hizo zinatamka kuwa klabu zinazoshiriki michuano ya CAF hazitaruhusiwa kuwa na mdhamini shindani wa mdhamini mkuu wa CAF. Kwa sasa mdhamini huyo ni 1xbet.
Mkataba huo wa jana una thamani ya shilingi bilioni 1.5.

Post a Comment