MSIBA MKUBWA MBINGA MJINI
Mama Messe Julius Mapunda, mjasiriamali maarufu mjini Mbinga, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana na kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa mji huu.
Mama Messe ni mmiliki wa jengo hili ambapo kuna klabu maarufu ya starehe ijulikanayo kwa jina la 24 Night Club, lililopo stendi mjini hapa.
Mamia ya waombolezaji walikutanika nyumbani kwa marehemu na kusababisha utaratibu wa kutoka katika stendi ya mabasi ya mjini hapa kuvurugika kwa muda. Nyumba ya marehemu ipo katika lango kuu la kutokea stendi na hivyo ilibidi mabasi ya abiria kutokea mlango wa kuingilia.
Anayedhaniwa kuwa binti ya marehemu akiangua kilio kikubwa wakati mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani tayari kwa kupelekwa kanisani kwa ibada.
Magari ya waombolezaji mbalimbali yakiwa yameegeshwa nyuma ya stendi.
Wajukuu wa marehemu
Ibada ya kumuombea marehemu ikiendelea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Alois mjini Mbinga.
Maandalizi ya mwisho yakiwa yanaendelea kuusubiri mwili katika Makaburi ya Kiwandani mjini Mbinga leo Alhamisi.

Post a Comment