TRESOR MPUTU ASTAAFU SOKA AAGA KWA MACHOZI TP MAZEMBE IKIMPIGA MTU 3-1

Tresor Mputu, mshambuliaji nyota na wa muda mrefu wa TP Mazembe, ametangaza kustaafu soka wakati timu yake ikishinda mabao 3-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho wikiendi iliyopita.

Mputu, aliyejiunga na TP Mazembe mwaka 2002, alimwaga machozi uwanjani wakati akiwaaga mashabiki wa timu hiyo, ambayo ilimpa mataji yote makubwa katika soka la Afrika.

Mputu, aliyecheza sambamba na nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta, amechukua taji la mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi ya Shirikisho, Chan na ligi ya ndani nchini DRC. Amestaafu akiwa na umri wa miaka 37.

No comments