MUINGEREZA ALIYEIUZIA UKRAINE MAGARI 100 YA KIVITA AKAUNTI YAKE YAFUNGWA

Raia mmoja wa Uingereza, ambaye amejikita katika kutengeneza magari ya kivita, na tayari alishauza magari zaidi ya 100 kwa Ukraine, iliyo vitani na Urusi, akaunti yake imefungwa na benki maarufu nchini humo, Bacrays.

Nick Meads, mwenye umri wa miaka 61, ambaye hutengeneza magari, vifaru na vifaa vingine vya kijeshi, amezuiliwa kuendelea kuitumia akaunti yake ya benki.

Muingereza huyo ambaye amekuwa akitengeneza zana za kivita kwa ruhusa ya mamlaka, amesema akaunti zake zote mbili, ya biashara na binafsi zitafungwa kuanzia Februari 20 mwaka huu.

Kutokana na uamuzi huo, ambao umefanywa baada ya miaka 40 ya kutumia akaunti hiyo, utamuathiri kibiashara na kibinafsi.




No comments