TETESI: FEI TOTO KULIPWA MILIONI 15 KWA MWEZI, KUREJEA JANGWANI BAADA YA MECHI YA TO MAZEMBE

Tetesi kutoka vyanzo mbalimbali na vilivyo karibu na uongozi wa Yanga na Feisal Salum Abdallah zinasema pande hizo mbili zimefikia makubaliano ya kuboresha mkataba wa Zanzibar Finest, na kwamba sasa atakuwa analamba shilingi milioni 15 kwa mwezi, mara nne zaidi ya awali.

Vyanzo hivyo vimesema, viongozi wa mabingwa wa kihistoria katika soka la Tanzania, walisafiri hadi kwenye marashi ya Karafuu, ambako waliketi na mchezaji huyo, mmoja kati ya viungo bora wazawa kwa sasa.

Katika kikao hicho cha kutumia zaidi busara kuliko sheria, ilikubaliwa kuuboresha mkataba wa mchezaji huyo wa zamani wa JKU, ambapo sasa atalipwa kama mshahara shilingi milioni 15 kwa mwezi.

Imeelezwa kuwa Fei Toto, kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kwa mashuti makali, atarejea Avic Town,ilipo kambi ya Yanga, mara baada ta mchezo wa pili wa michuano ya Kombe la Shirikisho Jumapili hii, dhidi ya TP Mazembe kutoka DRC.

No comments