NI VITA YA URUSI NA ULAYA, SI UKRAINE

Februali 24 mwaka huu,Putin ambaye ni rais wa Russia, atatimiza mwaka mmoja tangu aanzishe mashabulizi dhidi ya Ukraine, moja kati ya nchi zilizozaliwa kutoka dola ya USSR, kufuatia mabadiliko ya Rais wa mwisho wa Urusi,Michael Gorvachev miaka ya 90.

Wakati dunia ikitega masikio kuona lini Russia itaibuka mshindi wa vita hivyo, jambo lililo wazi ni kuwa 9vita hivi sio dhidi ya Ukraine, bali Ulaya naMarekani.

Mataifa yanayounda Umoja wa Kujihami Kijeshi ya Ulaya maarufu kama NATO, yamekua toka mwanzo yakitoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine, ambayo iliiudhi Klemlin, Ikulu ya Moscow, baada ya mpango wake wa kujiunga na jumuia hiyo ya Ulaya.

Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na mataifa mengine yamekua yakitoa misaada ya zana za kijeshi kwa Ukraine, ili ikabiliane na Rusisia ambayo takwimu za kijeshi zinaonyesha bado ina nguvu kubwa ndani ya uwanja wa mapambano.

Kitu cha muhimu na msingi kwa dunia ni kutambua kuwa Russia haitashindwa vita hivi, bali kuna janga linaandaliwa ili kuidhuru dunia. Putin anasogeza meli za kivita zenye silaha za nyuklia kule Ukraine, akijaribu kuwaonya washirika kuacha kuisaidia nchi hiyo.

Jambo pekee ambalo Putin, kachero wa zamani wa KGB, shirika la ujasusi la Urusi anaweza kufanya ili asishindwe ni kutumia nyuklia.

Akiamua kufanya hivi, madhara sio kwa wananchi wa Ukraine tu, bali dunia nzima.

No comments