AOKOTA DOLA MILIONI NNE WAKATI AKIOKOA WALIOFUKIWA UTURUKI, AZIKABIDHI POLISI
Mmoja wa watu walio katika timu ya uokoaji katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki, Muhammad Ozil Oslo ameokota fedha, dola za Marekani milioni nne, sawa na shilingi za Kitanzania bilioni tano.
Katika kutii kiapo na uaminifu uliotukuka, muokoaji huyo alizikabidhi fedha hizo kwa polisi ili wawatafute wenye zao wapate kurejeshewa.
Hadi asubuhi ya leo, jumla ya watu 41,000 wamethibitishwa kupoteza maisha kutokana na kadhia hiyo katika nchi za Uturuki na Syria.

Post a Comment