RAIS SAMIA ANUNUA KILA BAO LA SIMBA, YANGA KWA MILIONI TANO

Rais Samia Suluhu Hassan, atanunua kwa shilingi milioni tano kwa kila bao ambalo tomu za Simba na Yanga zitafunga wakati wa mechi zao za kimataifa wikiendi hii.

Simba itacheza mechi yake Jumamosi hii katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco saa moja usiku na watani wao Yanga, wataikaribisha TP Mazembe kwenye uwanja na muda huohuo siku ya Jumapili.

Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa aliwaambia waandishi muda mchache uliopita kuwa hiyo ni moja ya hamasa ya kutakatimu hizo za Tanzania kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Simba inayocheza Ligi ya Mabingwa Afrika, ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Horoya ugenini nchini Guinea wakati Yanga, walio katika michuano ya Kombe la Shirikisho, nayo ilichapwa mabao 2-0 dhidi ya US Monastr ya Tunisia.

No comments