DC ATAKA VIJANA WALIOHITIMU KOZI KUPEWA TENDA

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo amezitaka mamlaka zinazohusika na barabara kuwapa kazi vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya ukandarasi ili waweze kujipatia kipato na kutoa ajira kwa watu wengine.

Akizungumza wakati wa mahafali ya mafunzo hayo yaliyochukua mwezi mmoja, DC Aziza alisema vijana hao kutoka vikundi vitatu, watakuwa ni chachu cha kuiajiri na kuajiri watu wengine kupitia kazi kama vile usafi wa mitaro, ukataji majani na usafi.



Aidha, aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kuwapa mikopo vijana hao ili waweze kununua vifaa vya kazi kwa ajili ya kazi za barabarani.



No comments