MAWAZIRI SASA KUJIELEZA NA KUJIBU MASWALI YA WANANCHI MUBASHARA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuanzia sasa wameandaa utaratibu maalum ambapo mawaziri na wataalamu wa wizara zao wataeleza mikakati yao live kupitia chaneli ya Maelezo News.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo, Msigwa alisema atakayekata utepe wa zoezi hilo ni Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye.

Alisema Waziri Nape ataanza na mada ya Utekelezwaji wa mradi wa anuani ya makazi na kwamba mijadala hiyo ya saa moja itarushwa kila Jumamosi kuanzia saa tatu usiku na wananchi wataruhusiwa kuuliza maswali ya papo kwa hapo.

Msigwa alifafanua kuwa lengo la mijadala hiyo ni katika ushirikishwaji wa wananchi na utendaji wa serikali yao.


No comments