MV MWANZA YAINGIZWA MAJINI, BONGE LA MELI AFRIKA MASHARIKI
Meli mpya, kubwa na kisasa MV Mwanza 'Hapa kazi tu', imeingizwa ndani ya maji katika bandari ya Mwanza Kusini, ujenzi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 82.
Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa amesema wakati wa zoezi la kiingiza meli hiyo yenye ghorofa nne na ambayo itakuwa na madaraja sita, imeundwa na kampuni kutoka Korea.
Alisema ujenzi huo utakapokamilika miezi michache ijayo, itaweza kubeba abiria 1200 na mizigo kiasi cha tani 400.
Meli hiyo iliyoanza kujengwa wakati wa uongozi wa hayati John Magufuli, itagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania, bilioni 106.
Itatoa huduma katika mikoa yote inayozunguka Ziwa Victoria na nchi jirani na mojawapo ya maeneo ndani ya meli hiyo ni sehemu maalum ya viongozi, burudani, vyakula na vinywaji.

Post a Comment