CHAMA AIUA SINGIDA BIGSTARS
Clatus Chota Chama, kiungo mwerevu wa Simba, usiku huu ameiwezesha timu yake ya Simba kuifunga Singida BigStars kwa mabao 3-1, katika moja kati ya mechi bora za NBC Plemier League msimu huu.
Chama, kiungo kipenzi cha mashabiki wa Msimbazi, alipiga faulo mbili zilizozaa mabao, la kwanza likifungwa na mshambuliaji Bareke na baadae, Saidoo Ntibanzikiza.
Katika kipindi cha pili, Pape Osman akashindilia bao la tatu, huku kiungo bora kabisa wa Singida, Mbrazil, Bruno Gomes akifunga bonge la bao la faulo kuipa SBS bao la kufutia machozi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa

Post a Comment