MNYETI APANDISHWA KIZIMBANI

Mbunge wa Misungwi, Alexander Mnyeti amesomewa Mashtaka Mahakamani kwa kosa la Matumizi mabaya ya madaraka.

Imesemwa Mahakamani Mbele ya Jaji John Kahyoza kwamba, Ndugu Mnyeti akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara aliinyang'anya Kitalu cha Uwindaji kampuni ya HSK SAFARIS LTD ya wilayani Simanjiro kinyume kabisa cha Sheria za Nchi na kuisababishia hasara kubwa.

Wakati akifanya unyang'anyi huo imetajwa kuwa alishirikiana na Belinda Sumari, anayetambulika kama Ofisa Mtendaji wa Kata ya Emboreet na Salehe Alamry ambaye hakutajwa cheo chake.

Mnyeti anatetewa na Wakili Kuwengwa Ndojekwa, ambaye ameiomba Mahakama ikubali Serikali ya Tanzania nayo iunganishwe kwenye kesi hiyo kwa vile alitenda unyang'anyi huo akiwa Mkuu wa Mkoa.


Bengal

JF-Expert Member
Bado mmoja sijamsikia ,akikokotwa kwa mahakama,anaye mjua amtaje🤔
900 Inapendeza zaidi

900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nitashanga hapa kama hapatatimia usemi wa kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake au kilammoja ashinde mechi yake,halafu utawasikia wahuni wakisema marehemu asitajwe, yaani nasema atatajwa sana na bado

No comments