HABARI PICHA MCHANGANYIKO
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), magari 14 na maboresho ya Jengo la Watu Mashuhuri katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja cha Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya USafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi magari 14 uliofanyika jijini Dar es Salaam.PICHA 4Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mussa Mbura (kulia), baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), magari 14 na maboresho ya Jengo la Watu Mashuhuri katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dkt. Ally Possi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (wa pili kulia), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja cha Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura (kushoto) wakikata utepe kuashiria kukamilika kwa maboresho ya Jengo la Watu Mashuhuri katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere

Post a Comment