MANDONGA ATAKA KUONANA NA DIAMOND
Bondia anayepata umaarufu kila kukicha, Mandonga Mtu Kazi, ameomba kukutana ana kwa ana na msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari, bila kusema nini hasa anataka kuteta na msanii huyo, Mandonga alisema anahitaji kuongea na mkali huyo ili aweze kutoa dukuduku lake.
Hata hivyo alidokeza kukerwa na kauli ya meneja wa msanii huyo, Sallam kitu ambacho huenda kikahusiana na ishu hiyo

Post a Comment