SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AUTILIA MASHAKA UDOKTA WA MENEJA. WA TIPTOP CONNECTION
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Atkson ameutiliia shaka udaktari wa mbunge wa CCM, Hamis Taletale aliyekuwa meneja wa kundi la muziki wa kizazi kipya la Tiptop Connection la Manzese jijini Dar es Salaam.
Taletale maarufu kama Babu Tale ambaye sasa ni miongoni mwa viongozi wa WCB, lebo ya msanii kinara nchini, Diamond Platnamz, alisema bungeni kuwa anataka atambuliwe kama dokta.
Spika Tulia, akionyesha kukerwa, alisema wazi kuwa heshima anayodai mbunge huyo wa chama chake ni ya kununua na haitoi picha nzuri kwa watoto wanaohimizwa kwenda shule, maana waanaonyeshwa kuwa pesa yaweza wapa heshima pasipo kufanya kazi kitaaluma au kijamii kwa kwa weledi uliotukuka.
Babu Tale ambaye hafahamiki kiwango chake cha elimu, ameushtua umma bsada ya kuongea bungeni leo, akitaka atambuliwe kama daktari wa heshima.

Post a Comment