JAKAYA KIKWETE ATAKA WASANII BONGO FLEVA KUMTOA OUT

Rais wa  awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewata wasanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, kumpa mialiko bila woga, kwani yeye atahudhuria kwa vile anapenda muziki mzuri.

Alitoa ombi hilo siku chache zilizopita wakati akiwa katika shoo ya uzinduzi wa albamu ya Marioo, The Kid You Know, iliyofanyika Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

JK ambaye licha ya kupenda muziki pia ni shabiki kindakindaki wa soka wa mabingwa wa kihistoria, alisema anaishi maisha magumu kidogo, kwani nyumba yake imezungukwa na ukuta mkubwa, kabla ya nyumba nyingine kuizunguka ile anayoishi.

Kwa ajili hiyo, alisema mialiko ya mara kwa mara ya wasanii ni muhimu kwake kwa kuwa itamfanya kuwa na mitoko ya usiku itakayomfanya avinjari kwani naye ni binadamu.

Mapenzi ya Jakaya katika muziki wa kizazi kipya yanarudisha kumbukumbu za yeye kuwahi kumsaidia msanii Rehema Chalamila Ray C kwenda katika kituo cha kuondoa uraibu wa matumizi ya madawa ya kulevya miaka ya 2010.

No comments