17 WAKABIDHIWA VYETI VYA UKANDARASI MBINGA

Wakufunzi 17 kutoka vikundi vitatu kutoka Halmashauri mbili za Wilaya ya Mbinga, jana walitunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Kozi maalum ya Ukarabati na Matengenezo ya Barabara kwa kutumia Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi.

Wakufunzi hao, wakiwemo wanawake sita, ambao walishiriki kozi hiyo ya mwezi mmoja, walikabidhiwa vyeti hivyo na Mkuu wa Wilaya Ya Mbinga,

Aziza Mangosongo.


 

Wakufunzi hao walipata mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICOT) ya jijini Mbeya.

ICOT iliwaleta wakufunzi wawili kuendesha kozi hiyo ambao ni Injinia Richard Kansimba na Donatha Kamwela ambao nao walikabidhiwa vyeti maalum vya kutambua mchango wao kutoka kwa DC Aziza.



Mkufunzi Donatha Kamwela akisoma risala mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti hivyo.

No comments