CAF YAWASILI KUIKAGUA SIMBA YA AFRICA SUPER LEAGUE
Wajumbe maalum kutoka Shirikisho la soka barani Africa (CAF) wamewasili nchini kwa ajili ya kuikagua Klabu ya Simba ambayo itashiriki michuano ya Africa Super League Agosti mwaka huu.
Baada ya kuwasili wajumbe hao walipokelewa na kushiriki kikao cha pamoja kutoka kwa viongozi wa Serikali, Shirikisho la Soka nchini TFF na klabu ya Simba yenyewe.
Baadhi ya viongozi hao walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Ally Mayai ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Michezo, Boniface Wambura kutoka TFF, Said Abdallah 'Try Again' na Murtaza Mangungu.

Post a Comment