UVCCM KUPANDA MITI MBUJI

Kuelekea kilele cha Sherehe ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapo Februari 5, Jumuia ya vijana ya chama hicho Wilaya ya Mbinga, kesho watasafi hadi Tarafa ya Mbuji kwa ajili ya shughuli mbalombali za kijamii, kubwa zaidi ikiwa ni kupanda miti.

Katibu Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Mbinga, Daniel Patson Nkoma ameiambia Ojuku Blog:

"Tunakwenda kufanya shughuli za kijamii wakati tunaelelea kuadhimisha miaka 46 ya CCM, mojawapo ya kazi tutakayoifanya ni kuandikisha wanachama wapya, kufanya usajili wa kielektroniki na kubwa zaidi ni upandaji miti.

"Tunategemea Kamati ya Utekelezaji na vijana kadhaa watashiriki, ni msafara utakaohusisha watu takribani 30," alisema Nkoma.

Nkoma alikuwa ni miongoni mwa vijana wanne waliogombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mbinga uliofanyika wiki iliyopita, nafasi ambayo ilichukuliwa na Herswida Komba.

No comments