SOKO LA MCHELE MBINGA LASHUKA, WAFANYABIASHARA WAFUNGUKA
Wafanyabiashara wa mchele Wilayani Mbinga, wamesema kuwa soko la bidhaa hiyo limekuwa gumu kutokana na kupanda kwa bei.
Wameiambia blogu hii kuwa kupanda huko kwa bei kunatokana na kuadimika kwa bidhaa hiyo kulikosababishwa na kuchelewa kwa mvua msimu uliopita.
Kijana Alex Onesmo ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara hiyo wilayani hapa, anasema bei za mwaka huu ni kubwa tofauti na msimu uliopita.
"Mchele hapa kilo moja ni kati ya 2500-3000 kutegemea na uzuri wake. Biashara ni ngumu kutokana na wateja kupungua, lakini hata hivyo tunashukuru riziki tunapata," alisema Alex.
Akizungumzia hali ya soko, alisema licha ya ugunu uliopo. lakini wanapata wateja hasa wa majumbani na magengeni, tofauti na watu kutoka nje ya wilaya.
"Wateja wetu wakubwa ni wenyeji, watu kutoka majumbani ndiyo wengi na wachache ni wafanyabiashara wa magengeni."

Post a Comment