MAHESABU YA YANGA YAKAMILIKA KWA WIKI BENJAMIN MKAPA
Wananchi wamefunga hesabu mwishoni mwa wiki hii, kwa kuipa bakora saba, timu ya Rhino Rangers katika mchezo wa michuano ya Azam Confidaration Cup, uliopigwa usiku huu pale Benjamin Mkapa Stadium.
Yanga, ambao ni mabingwa wa kombe hilo, wakiwa pia ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, walionyesha kiwango kikubwa cha soko kiasi cha kuondoa kabisa ushindani katika mechi hiyo.
Hadi mapumziko, vinara hao wa Ligi Kuu walishampa mtu bao tano, au kama watoto wa mjini wanavyosema, walimpiga mkono!!!

Post a Comment