MAREKANI YATAHADHARISHA SHAMBULIO LA KIGAIDI TANZANIA
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari ya kuwepo kwa viashiria vya shambulio la kigaidi nchini Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo imesema shambulio hilo litawalenga raia wa Ulaya na Marekani na kwamba maeneo yanayolengwa ni mahoteli makubwa, maduka makubwa(Malls), vituo vya polisi na maeneo ya ibada.
Raia wa nchi za Magharibi na Marekani wametakiwa kuwa na tahadhari.

Post a Comment