MAREJEO UVHAGUZI UVCCM MBINGA LEO
Marejeo ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Mbinga yanafanyika leo katika Ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC).
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mbinga, Mohamed Salmin, ameiambia Ojuku Blog kwamba jumla ya vijana wanne watasimama mbele ya wajumbe zaidi ya 600 ili kunadi sera zao kuitafuta nafasi ya Mwenyekiti ambayo ipo wazi.
Aliwataja vijana hao wanne waliopatikana katika mchujo wa majina 15, uliofanywa na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma kuwa ni msichana pekee, Heriswida Sines Komba, Daniel Patson Nkoma, John Charles Mbawala na Isiaka Mohamed Rajab.
Awali, uchaguzi huo ulifanyika kwa mujibu wa kalenda Septemba 23 mwaka jana ambapo Daniel Patson Nkoma alitangazwa mshindi, lakini baadae matokeo hayo yalitenguliwa na ngazi za juu za chama kwa kuwa mshindi huyo hakupata kura zaidi ya nusu kama kanuni zinavyoelekeza.

Post a Comment