MAREKANI YAITANGAZA WAGNER MAGAIDI
Kundi la wapiganaji la Wagner linalopigana sambamba na askari wa Russia nchini Ukraine, limetangazwa na Marekani kuwa kundi la kihalifu.
Ikulu ya Marekani imesema kundi hilo linalofadhiliwa na rafiki mkubwa wa rais wa Russia, linahusisha miongoni mwa wapiganaji wake wakiwemo wafungwa.
Kundi hilo linadaiwa pia kushiriki mapigano katika nchi za Syria, Libya na Jamhuri ya Afrika ya kati.
Katikati ya wiki hii ziliripotiwa taarifa zilizpdai raia mmoja wa Tanzania kuuawa katika mapigano akilipiganoa kundi hilo.

Post a Comment