KOBE ALIVYOMSHANGAA RONALDINHO

Marehemu Kobe Braynt, mcheza mpira wa kikapu bora zaidi nchini Marekani baada ya Air Jordan, aliwahi kukutana na mtundu wa soka duniani, Ronaldonho Gaucho, ambaye amachukuliwa kama binadamu aliyekuwa na uwezo wa kuuchezea zaidi mpira akiwa uwanjani.

Wakati wawili hao wakitawala enzi katika michezo walipokutana, Ronaldinho alimwambia Mmarekani huyo kuwa anataka akamtambulishe kwa mwanasoka bora zaidi wa soka wa muda wote.

Kobe akashangaa, akamuuliza, kuna mchezaji bora wa soka zaidi yako? Yule Mbrazil, ambaye sura yake imetawaliwa na tabasamu muda wote, akamwambua..

Yes, yupo dogo mmoja anajua na nina uhakika atakuwa mchezaji bora wa dunia wa muda wote, anaitwa Lionel Messi.

Wakati hao miamba wanaongea, kijana huyo wa Kiajentina alikuwa na umri wa miaka 17 tu. 


No comments