JOKETI, GONDWE WAONDOLEWA DAR

Joketi Mwegelo na Godwin Gondwe wanasiasa vijana waliokuwa wakuu wa wilaya za Temeke na Kinondoni jijini Dar wa Salaam, wamehamishwa kufuatia mabadiliko makubwa ya nafasi za wakuu wa wilaya yaliyofanywa na Rais Sanja Suluhu Hassama leo.

Kwa niujibu wa taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais Ikulu, Zuhura Yunus, Rais amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 37, akawahamisha 48 na kuwaacha 55 katika vituo vyao vilevile vya swali.

Watu wengine maarufu waliohamishwa katika vituo vyao vya swali ni pamoja na Halima Abdallah Bulembo aliyetolewa Kigamboni na kupelekwa Muheza, Kherry Denis James ambaye amepelekwa Mbulu akiondolewa Ubungo. Aidha, Moses Ma hali aliyekuwa akiiongoza wilaya ya Mkalama, sasa atafanya hivyo katika wilaya ya Bukoba.

Rais pia amemhamisha Joshua Nassari kutoka Numda na kumpeleka wilayani Irambi huku Albert Msando akipelekwa Handeni kutokea Morogoro. 

No comments