FRED LOWASA ATAKA BABA YAKE AENZIWE
Mtoto wa Waziri Mkuu wa kwanza katika serikali ya awamu ya nne, Edward Lowassa aitwae Fred, amewataka watendaji wa wilaya ya Monduli kuenzi mawazo ya baba yake ambaye ndiye muasisi wa shule za kata nchini.
Fred ambaye ni Mbunge wa jimbo la Monduli, ambalo baba yake alilihudumu kwa wadhifa huo kwa miaka mingi, alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza mwaka huu.
Aliwataka walimu na watendaji wengine wa elimu jimboni humo kuwatendea haki wanafunzi hao kwa kuwapa elimu bora na mahitaji ya msingi kama alivyoasisi baba yake.
Edward Lowasa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jakaya Kikwete aliyesimamia uanzishwaji wa shule za sekondari za kata nchi nzima zilizoanza miaka ya 2005_2010.
Lowasa alijiuzulu nafasi hiyo baada ya kuwajibika kutokana na kashfa maarufu ya Richmond na hivyo kurithiwa na Mizengo Pinda.

Post a Comment