BASHE AWAASA WATANZANIA KUACHANA NA KILIMO CHA WHATSAPP

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amewataka watanzania kuachana na dhama ya kilimo cha kutumia mitandao ya simu na badala yake, amewataka kwenda shambani.

"Hakuna shortcut katika kilimo. mtu anakuambia eti toa milooni mbili baada ya miezi mitatu utapata milioni kumi, hakuna hilo jambo, nenda mwenyewe shambani."

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus amesema serikali imeongeza bajeti ya kilimo mara tatu zaidi ya ilivyokuwa mwaka jama.

No comments