TALIBAN WAOMBA KUTAMBULIWA KIMATAIFA, WAUA HARUSINI

WAKATI wanamgambo wanaotawala
Afghanistan wa Taliban wakiomba Jumuia za kimataifa kuwatambua na kuwapa
misaada, watu watatu waliobeba silaha ambao wamejitambulisha kuwa ni Wanamgambo
wa Taliban wamevamia harusini na kuamuru Muziki usimame kisha kuwaua Watu
watatu na kuwajeruhi wengine kadhaa huku wakisema sababu ya kufanya hivyo ni
kuzuia shughuli za Muziki ambazo zimepigwa marufuku nchini Afighanistan.
Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema Serikali haijahusika
na mauaji hayo na kusema washambuliaji wawili kati ya watatu wamekamatwa na wanashikiliwa
"Mtu akifanya mauaji hata kama ni Askari wetu tunamuona Mhalifu na
tutamfikisha Mahakamani ili aadhibiwe"
Wanamgambo wa Taliban walitangaza kuzuia shughuli zote za
Muziki baada ya kuchukua madaraka nchini Afighanistan wakisema ni kinyume na maadili
ya Kiislamu.

Post a Comment