SIMBACHAWENE AWATAKA WAMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA KUZISALIMISHA KWA HIARI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani George
Simbachawene ametoa siku 30 kuanzia November 01,2021 hadi November 30,2021 kwa
Watu wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha silaha zao na
amesititiza kuwa watakaotii agizo hawatochukuliwa hatua.
"Natoa msamaha na usalimishaji wa silaha kwa wanaomiliki
kinyume na sheria na ninawataka kuzisalimisha silaha hizo katika Vituo vyote
vya Polisi, Ofisi za Serikali za Mitaa na kwa Watendaji wa Kata kuanzia saa 2
asubuhi hadi saa 10 jioni, Wahusika hawatoshtakiwa endapo watazisalimisha
silaha hizo haramu kwa hiari na kwa muda uliopangwa"——— Simbachawene
"Baada ya muda uliowekwa kupita msako mkali utafanyika
kwa Nchi nzima ili kuwakamata wote waliokaidi nafasi ya msamaha waliyopewa,
zoezi hili litakuwa ni Mwezi November tu na atakayeshindwa kuwasilisha silaha
ndani ya muda uliotamkwa atachukuliwa kama Mtuhumiwa"——— Simbachawene

Post a Comment