SIMBA KUACHANA NA MAKOCHA WA KIZUNGU

CEO wa Klabu ya Simba,Barbara
Gonzalez amesema malengo ya Klabu ya Simba kwa Sasa ni kumwajiri Kocha wa
Ki-Afrika na sio mzungu ili kuziba nafasi ya Didier Gomes ambaye waliachana
naye hivi karibuni.
Inaelezwa kuwa Simba ipo kwenye
mipango ya kumchukua Kocha Msaidizi wa Mamelodi Sundowns,Rulani Mokwena kuwa
Kocha Mkuu wao.
"Suala la kocha halihitaji
kukurupuka, kwani tunaweza kumpata mwenye wasifu mkubwa lakini akashindwa
kutibu matatizo yaliyopo katika kikosi cha Simba na shida ikabaki pale pale,”
“Kama atakuwa Mokwena au
mwingine hilo litajulikana ndani ya muda mfupi, lakini malengo ya klabu ni
kumpata kocha kutoka Afrika na si Mzungu kama iliyetoka"
“Tunaweza kumpata kocha wa
Afrika ambaye tunamuhitaji na wasifu wake usiwe mkubwa na akaweza kuisaidia
timu kufikia malengo yake kwani atakuwa na kiu ya mafanikio na tutadumu naye
kwa muda mrefu"
“Angalia klabu kama Chelsea wakati wanamchukua Thomas Tuchel wengi hawakuwa na imani naye, ila baada ya muda mfupi ameifanya timu kucheza vizuri na kushinda ubingwa wa Ulaya.”

Post a Comment