SERIKALI YATAMBUA UWEPO WA MWANASOKA KINDA ULAYA

WAKATI Serikali ikiwa na mpango wa
kujenga Sports Arena Dar es salaam na Dodoma, vituo vya michezo na hivyo
kuhamasisha sekta binafsi, imesema inatambua uwepo wa mwanasoka kinda, Baraka
Seif barani Ulaya kwa majaribio.
“Tunae Bwana Mdogo hivi ninavyozungumza anapita Ulaya huko,
anaitwa Baraka Seif ana miaka saba tu tayari ameshakwenda Uholanzi, Ubelgiji
anakwenda sasa Hispania, kituo chake kile kinaitwa Magnet Academy kipo hapa
Tanzania kinafanya vizuri, Baraka ni juhudi binafsi za Mzazi wake tunampongeza
sana na kituo chake kinachomuandaa tunakipongeza,” amesema Gerson Msigwa,
Msemaji wa Serikali ya Tanzania.

Post a Comment