KAMPENI YA CHANJO SASA HADI VIJIJINI

WAKATI serikali ikiendelea
kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya ugonjwa wa corona hasa sehemu za mijini,
kampeni kubwa inayofanyika sasa ni kupeleka chanjo vijijini ili Watanzania
wengi waweze kuipata.
Msemaji mkuu wa serikali, Gerson
Msigwa amesema mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa Oktoba 2021 kutakuwa
na “Wiki ya Uchanjaji” ambapo viongozi nchi nzima watashiriki moja kwa moja
kwenye wiki hiyo kuhakikisha watanzania wengi wanapata chanjo ili kuepuka
madhara ya ugonjwa huo.

Post a Comment