BUNGE LASITISHA SHUGHULI ZAKE KUJADILI BEI NDOGO YA MAHINDI KWA WAKULIMA
BUNGE limesitisha kwa muda
shughuli zake za leo ili kujadili changamoto ya bei duni inayowakumba wakulima
wa mahindi nchini. Wabunge wameeleza kutoridhishwa na bei ndogo ya mahindi, bei
ghali ya mbolea hivyo wameitaka Serikali kuiongeza hela NFRA ili inunue mahindi
kwa wakulima.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda amekiri uwepo wa tatizo la bei ndogo ya mahindi.
Ameeleza kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kushughulikia suala hilo
ambapo ameahidi kuwa kabla ya Bunge kuhitimishwa hapo kesho Serikali itatoa
tamko bungeni kuhusu hatua ilizochukua.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali imesikia kilio na Serikali
na kupitia NFRA ilianza kununua mahindi kwa wakulima lakini imegundua kuwa
uzalishaji wa mwaka huu ni mkubwa na Serikali imefanya mazungumzo na mataifa
jirani ili kununua mahindi hapa nchini.

Post a Comment