RAIS WA ZANZIBAR AWAPA MASHAMBA WAKULIMA WETE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi ametoa idhini ya mashamba ya karafuu
maarufu kama mashamba ya EKA kupewa Wakulima na Wamiliki wanaoyahudumia badala
ya mfumo wa sasa wa Serikali kuwakodishia.
Akizungumza na Wananchi kwenye ziara yake inayoendelea
Kisiwani Pemba Dr. Mwinyi amesema Serikali imefikia uamuzi huo baada ya kuona
hakuna haja ya kuendelea na mfumo wa zamani wa kuwakodishia mashamba Wakulima
ili hali Serikali haiyahudumii.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya Wete-Konde Mkoa wa Kaskazini
Pemba, Rais Mwinyi amesema Serikali imeshatoa shilingi milioni mia saba (700)
kwa ajili ya kuwalipa fidia Wakazi walioondolewa kupisha ujenzi wa barabara
hiyo.
Jana September 1 2021 Rais Mwinyi amekua Rais wa pili wa
Zanzibar baada ya Hayati Abeid Aman Karume kutembelea Kijiji cha Mleteeni
kilichopo Wete Jimbo la Mtambwe Kaskazini Pemba ambacho hakijawahi kutembelewa
na Kiongozi yeyote wa juu tangu mwaka 1969.
Rais anaendelea na ziara yake leo Kisiwani
Pemba kwa kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na Wananchi katika Mkoa wa
Kusini Pemba ambapo atatembelea Wilaya ya Chakechake.

Post a Comment