RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIRI WAHISANI KUSITISHA MISAADA

RAIS Samia Suluhu Hassan amewaambia watanzania kwa sasa
wahisani hawaleti misaada nchini, badala yake wanataka biashara ili kugawana
faida
Amesema kwa sababu hiyo ni lazima tujinyang'anye wenyewe ili
kufadhili miradi yetu.
Amesema hayo alipokuwa Tegeta akisalimia wananchi akiwa
katika safari ya kuelekea Bagamoyo kutengeneza filamu ya kuitangaza Tanzania
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amesema mikopo ina riba kubwa
na misaada imepungua, hivyo ni lazima wananchi kujichanga ili kujenga nchi
Amesema ni heri kuchukua mikopo kidogo kufadhili miradi
mikubwa kama ya reli na umeme. Amesema hayo alipokuwa Zinga mkoani Pwani
akielekea Bagamoyo.

Post a Comment