POLISI WALALAMIKIWA KUNYANYASA WANAWAKE KINGONO HANDENI

WAKATI bado kukiwa na hisia tofauti
juu ya ufanisi wa maadili na utendaji kazi kwa weledi wa baadhi ya askari
Polisi, wanawake wilayani Handeni wamelalamika kuwa wananyanyaswa kingono na
vijana hao wa IGP Simon Siro.
Mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya,
Sirieli Mchembe, wananchi hao wamesema unyanyasi wa baadhi ya Polisi
hauvumiliki.
Mwanamke mmoja alisema..,. "Kuna Askari wakija humu
ndani 'night club' wanatushika bila ridhaa yetu.. wanataka wanawake kilazima,
akiona mwanamke anamkataa anamtafutia sababu anamkamata kwenda kumlaza selo"
Naye kijana wa kiume akamwagika... "Wakija humu ndani
wanatufanyia jinsi wanavyotaka wao, demu wako mzuri anachukuliwa ukizingua
unapigwa"
Mwananchi mwigine aliyesimama alisema "Anakuja na
bunduki anaingia ndani mpaka Club humo ndani anachukua Mtoto wa kike anafanya
vile anavyotaka, hata mimi siku hiyo nilikua natoka safari roho iliniuma na
ukiangalia gari ya Polisi imepaki pale, anafanya unyama"
Baada ya Malalamiko hayo ya Wananchi Mkuu wa Wilaya Sirieli
Mchembe alitoa tamko la Serikali huku akielezea tukio la hivi karibuni la
mabinti wawili kupigwa na askari hao ndani ya moja ya kumbi za starehe zilizopo
Wilayani Handeni jambo lililopelekea kuitisha mkutano nje ya ukumbi huo huku kura
za siri zikipigwa kuwataja askari hao.
"Hakuna askari mwenye mamlaka ya kumgusa au kumchezea mwanamke
maeneo yake bila kibali chake, cheo cha mtu hakihusiani na mwili wa mtu, mabinti
wale watakuja hapa mtaona mmoja mpaka sasa hivi jicho limevimba wamepigwa
mangumi ya hatari, Mimi kama DC Mwanamke unyanyasaji wa kijinsia Handeni hapana."

Post a Comment