MAHUSIANO: HAKUNA MUME/MKE WA MTU DUNIANI

WIKI chache
zilizopita, nilikuwa nyumbani kwetu kijijini Mkumbi, wilaya ya Mbinga mkoani
Ruvuma. Ndiyo asili yetu, nilizaliwa kule, nimesomea kule hatua za awali na
nzuri zaidi, ninajua kuzungumza lugha ya kwetu, KIMATENGO.
Wamatengo kiasili
ni watu wakarimu na ni wengi jijini Dar es Salkaam na mikoa mingine. Uzuri
mwingine pia juu yao, ni miongoni mwa makabila ambayo yamejitahidi kuwapeleka
shule watoto wao, kiasi kwamba tunao ndugu zetu wengi tu katika nafasi
mbalimbali kubwa serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata taasisi binafsi.
Nikiwa hapa Dar
ninao ndugu, jamaa na marafiki tunaotokea wote huko, kiasi ambacho tumeunda
hadi umoja wa wamatengo. Sasa nikasafiri hadi kule, nikafika kijijini kwetu
salama salimini.
Usiku wa saa mbili,
simu yangu ikaingia ujumbe wa kunisalimia, nikaujibu na baadae ukaendelea
kunijulia hali ya safari iliyosababisha niulize mwenzangu alikuwa ni nani.
Akajitambulisha.
Asee, ni mmoja kati ya akina dada wamatengo ninayefahamiana naye tangu Dar,
akinifahamisha kuwa yeye alikuwa Mbinga mjini na amepata taarifa kutoka kwa
mmoja wa wanakijiji wenzangu juu ya ujio wangu. Nilifurahi sana.
Ni kitambo kidogo
tulikuwa hatujaonana. Tulichat kwa muda mwingi, akinifahamisha kuwa alikuwa
amehama jijini Dar na kuanzisha maisha Mbinga, akiwa ameolewa.
Baadaye,
akanikaribisha kumtembelea hapo mjini, angalau tupate mbili tatu maana anajua
mimi ni mtu wa bwax.
Kiutani,
nikamwambia ninaogopa mwaliko huo kwa sababu yeye tayari ni mke wa mtu na kama
waswahili wanavyosema, mke wa mtu sumu!
Huwezi kuamini,
pengine naye kiutani akaniambia, hakuna kitu kama hicho duniani, hakuna mke
wala mume wa mtu!
Of coz nilijua ni
utani, ambao hata hivyo baadaye, nikaupa nafasi ya kuutafakari akilini mwangu.
Tafakuri yangu ilitembea kufikia matukio mbalimbali tunayokutana nayo katika
maisha yetu ya kila siku hasa kwa wanandoa, wenye uhusiano, wachumba na hata
vijana wanaotafuta wenza wao wa kushare maisha!
To be honest, yule
mdada alikuwa sahihi. Unabisha? Ninasimama naye kwa mifano kadhaa michache
lakini yenye kufikirisha.
Kwanza, waswahili,
tuna kawaida ya kupenda kujidanganya. Acha kudanganyana, ni kujidanganya, yaani
wewe mwenyewe unajiapiza vitu vya uongo ili hali nafsi yako inafahamu kuwa ni
uongo.
Tuanze kwako
mwenyewe. Mimi nataka niamini kuwa wewe una umri unaoanzia miaka 18. Hebu
iambie nafsi yako, uhusiano uliopo hivi sasa ni wa ngapi tangu uanze utundu?
Simaanishi kuwa
wote ni waongo. La hasha, wapo wakweli, tena wakweli kabisa, lakini tukisema
tuwakague, trust me, kama ile treni ya Kigoma imejaza watu kibao, wenye mtu
mmoja katika maisha yao ya uhusiano, ni mmoja au wawili!
Nimeandika habari
za udaku kwa miaka kadhaa. Katika mojawapo ya habari nilizowahi kukutana nazo,
ni binti wa mchungaji kukutwa akiwa na ugonjwa wa ukimwi, baada ya jamii
iliyomzunguka kuamini kuwa hakuwa mtundu. Siyo tu hakuonekana akiwa na mtu,
lakini hata tabia zake zilishabihiana na dhana ya watu juu ya utakatifu wake.
Na siyo kwamba aliupata ugonjwa huo kwa kurithi, no, kuna jibaba lilikuwa
linatoka naye!
Maisha yetu ya
uhusiano yanapitia maeneo mengi sana hadi tunapokuja kuamua kuoa au kuolewa.
Huko nyuma, tunakuwa tumeacha watu wetu shule za msingi tulizosoma, sekondari,
vyuo na pengine miji tuliyohama.
Unapokuja kukutana
naye miaka kadhaa mbele, aina flan hivi ya dhambi ya asili inatukabili. Unaona
kama vile si kitu kwa vile uliwahi kuwa naye labda au hata kama aliwahi
kukutaka zamani mkiwa kwa mfano Singida, leo mmekutana Mtwara, unaona Why
uendelee kumbania?
Lakini ukiacha
hivyo, maisha yetu pia ya ndoa na uhusiano yana mazonge mengi. Kuna wanandoa
hawaongei kwa sababu ya madhila mbalimbali. Baadhi hudhani kwa kushiriki tendo
na mtu wa nje ni tiba!
Ndoa na uhusiano
wetu pia imekuwa kama kichaka cha kuficha maovu yetu. Mtu atakuwa mkali na
kusema yeye ni mke au mume wa mtu kwa mtu ambaye nafsi yake haimpendi, lakini
pale anapokuwa dhaifu, ni rahisi, rahisi mno kuisaliti ndoa au uhusiano wake.
Ninawafahamu wake
za watu wengi, wengine ni wake wa marafiki zangu, lakini wanashiriki mchezo huu
mchafu. Mimi pia nina mke, na naamini wapo rafiki zangu wanamuona akifanya
ndivyo sivyo. Wanaume ndiyo kabisaaaaaaa, hawafai hata kidogo.
Kwa kuwa wengi wetu
tuna udhaifu huu wa kibinadamu, jambo la msingi kulikumbuka ni kutunza heshima,
yako na ya mwenzio. Jitahidi kadiri unavyoweza kusaliti kwa staha. Nenda mbali
na unapoishi, jitahidi kushiriki na mtu asiyemjua mwenza wako na cha msingi, TUMIA KINGA!

Post a Comment