LA LIGA YAIZUIA BARCELONA KUMUENZI LIONEL MESSI

MASHABIKI na hata viongozi wa Barcelona
walitamani kuistaafisha jezi yao namba 10 kwa heshima ya nahodha wao
aliyeondoka, Lionel Messi.
Lakini sheria na kanuni za La
Liga zimewazuia kufanya hivyo.
Sheria hizo zinasema kila timu
ya La Liga inapaswa kusajili wachezaji wasiozidi 25 wenye namba kuanzia 1 hadi
25.
Lazima kuwe na makipa wasiozidi
watatu na watavaa jezi namba 1, namba 13 na namba 25.
Endapo kuna mchezaji kutoka timu
ya akiba (Timu
anatakiwa kutumika,
basi apewe jezi kuanzia 26 hadi 50.
Kwa hiyo endapo wangeistaafisha,
wangetakiwa kusajili wachezaji 24 tu, jambo ambalo lingekuwa tatizo kwao kwani
wangekuwa na kikosi chembamba.
Hii imewalazimu kuendelea
kuitumia jezi hiyo na sasa wamempa kijana kutoka akademi ya La Masia, Ansu
Fati.
Barcelona ni kama wana mkosi na
sheria za La Liga. Kisa cha kuondoka Lionel Messi ni sheria hizo hizo la La
Liga ambazo zinakataza timu kutumia zaidi ya asilimia 70 ya pato lake kulipa
mishahara.
Wafuatao ni wachezaji waliovaa
jezi namba 10 ya Barcelona ndani ya miaka 40 na ushei, iliyopita.
1978/1979 Juan Manuel
Asensi
1982/1984 Diego Maradona
1989/1990 Robert
1991/1992 Pep Guardiola
1991/1992 Richard Witschge
1993/1994 Hristo Stoichkov
1993/1994 -
1994/1995 Romário
1995/1996 LluÃs Carreras
1995/1996 Roger GarcÃa
1996/1997 -
1998/1999 Giovanni
1999/2000 Jari Litmanen
2000/2001 -
2001/2002 Rivaldo
2002/2003 Juan Riquelme
2003/2004 -
2007/2008 Ronaldinho
2008/2009- 2020/2021 Lionel
Messi
2021/2022 - Ansu Fati

Post a Comment