WANAJESHI 13 WA MAREKANI WALIPULIWA AFGHANISTAN



In this image provided by the U.S. Marine Corps, a Canadian coalition forces member walks through an evacuation control checkpoint during ongoing evacuations at Hamid Karzai International Airport in Kabul on Tuesday, August 24.


WANAJESHI 13 wa Marekani wameripotiwa kupoteza maisha katiuka shambulio la bomu lililofanyika katika mji mkuu wa Kabul, huko Afghanistan karibu na uwanja wa ndege.

Rais Joe Biden amesema Marekani itaendelea kuwaondoa watu Kabul licha ya shambulio lililosababisha vifo vya wanajeshi hao. Kwa mujibu wa Kituo cha Al Jazeera, raia wapatao 72 wamepoteza maisha.

Ameahidi kulipiza kisasi kufuatia kitendo hicho hawatosahau wala kusamehe na wahusika watasakwa. Licha ya kutolewa tahadhari ya kutokea shambulio, idadi kubwa ya watu walikusanyika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kabul wakitumaini kuruhusiwa kupanda Ndege.

Hadi sasa zaidi ya watu 100,000 wameshaondolewa Kabul wakiwemo 66,000 kutoka Marekani.



No comments