BEKI WA MAN CITY AFIKISHWA KORTINI KWA UBAKAJI


Footballer Benjamin Mendy arrives at Chester Magistrates Court today under police escort


 BEKI nyota wa Manchester City, Benjamin Mendy, 27, amefikishwa mahakamani leo akiwa amepakizwa katika karandinga ya polisi kujibu tuhuba za ubakaji na udhalilishaji wanawake.

Mlinzi huyo aliyejiunga kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 52 miaka minne iliyopita, anadaiwa kuwabaka wanawake watatu katika kipindi cha miezi kumi iliyopita, ndani ya jumba lake la kifahari lenye thamani ya paundi milioni 5.

Benjamin Mendy is pictured on August 12 out with his teammates at The Ivy in Manchester

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa anayelipwa paundi 90,000 kwa wiki, amesimamishwa na klabu yake kwa sasa.

Mwanasoka huyo aliwasili kortini Chester akiwa katika gari la magereza asubuhi ya leo.

Chanzo: Daily Mail

No comments