MWANDOSYA ASHAURI JAMII KUBADILIKA


Prof. Mark Mwandosya – Naturenews.africa

MWANASIASA mkongwe nchini, Mark Mwandosya, ameitaka jamii ya Kitanzania kubadilika, kwa kuacha tabia ya kuchangiana ndoa pekee na badala yake, kuchangiana pia katika masuala muhimu kama vile ada za shule kwa watoto wao.

Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa facebook, Mwandosya, aliyepata kuwania ridhaa ya chama chake (CCM) ili awe mgombea wake wa urais, aliandika....

Inaweza kuwa picha ya maandishi yanayosema 'Mark J. Mwandosya @MarkMwandosya Rafiki ameniomba msaada.Kijana Kijana wake amepata nafasi chuo kikuu anahitaji ada.Nimemuuliza ingekuwaje kijana angekuwa aoa?” wangeunda kamati.Nimeshauri wafanye,waorodheshe marafiki, mimi nikiwemo,i kama ilivyo harusi tuchangie.Kusiwe na kuvunja kamati.Katika li,Tubadilike.'





No comments