CAF WATOA ORODHA YA VIWANGO AFRIKA

SHIRIKISHO la soka barani Afrika, limetoa orodha ya viwanbgo vya soka vya klabu ambapo wakongwe wawili wa Tanzania wametofautiana sana nafasi.
Orodha hiyo iliyoongozwa na Al
Ahyl ya Misri inaonyesha kuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi
ya Mabingwa msimu uliopita, Simba wameshika nafasi ya 14 wakati mabingwa wa
kihistoria, Yanga wapo katika nafasi ya 56.
Orodha hiyo inaonyesha Simba ikiwa ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki huku Wananchi wakishika nafasi ya nne, nyuma ya Gor Mahia ya Kenya na KCCA ya Uganda.


Post a Comment