BAADA YA KUMKOSA KANE, MAN CITRY WAMTAKA RONALDO

MABINGWA wa soka wa
England, Manchester City, wamempa ofa mshambuliaji wa Juventus, Cristiano
Ronaldo ya mkataba wa miaka miwili wa malipo ya pauni 230,000 kwa wiki, lakini
wamekataa kuilipa timu yake ada ya uhamisho, baada ya Pep Guadiola kushindwa
kumpata strika wa Spurs, Harry Kane
Mfungaji huyo wa Spurs
aliuthibitisha Jumatano hii kuwa atabakia katika klabu yake.
Kikosi hicho cha Pep
Guardiola kilimfukuzia mshambuliaji huyo wa Tottenham na nahodha wa England kwa
msimu mzima, lakini fowadi huyo anayetajwa kuwa na thamani ya paundi milioni
150 alisema ana uhakika wa asilimia mia moja wa kubakia Spurs kwa msimu ujao.
Kwa kumkosa Kane,
ina maana City ina watu wachache mbele baada ya kuondoka kwa Sergio Aguero. Gabriel
Jesus ndiye mshambuliaji pekee wa kati ingawa wakati mwingine hucheza pembeni
huku Ferran Torres na Liam Delap wakiweza pia kutumika.

Post a Comment